Wachezaji
wa Timu ya Simba na baadhi ya viongozi wao wakipozi na kombe lao baada
ya kukabidhiwa kwa kuifunga Timu ya Yanga Mabao 3-1 katika mchezo wa
Nani Mtani Jembe, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
jioni ya leo.Mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Tambwe mawili na
Ramadhan Singano huku la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Emmanuel
Okwi.Picha zote na Othman Michuzi.
Meneja
wa Yanga, Afidh Ally akipokea mfano wa hundi ya zaidi sh. 98 milioni
Kwa kuibuka washindi katika shindano la Nani Mtani Jembe kwa kupata kura
nyingi katika unywaji wa bia ya Kilimanjaro.
Hundi ya Simba ilisomeka hivi pamoja na Ushindi Mkubwa walioupata dhidi ya wapinzani wao.
Mgeni
Rasmi katika Mchezo huo,Waziri wa Sheria na Katiba,Mh. Mathias Chikawe
akikabidhi Kombe la Ushindi wa Nani Mtani Jembe kwa Nahodha wa Timu ya
Simba mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo jioni hii kwenye Uwanja wa
Taifa,Jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Timu ya Yanga,Mrisho Ngassa (17),akiwa mpiga chenga ya Mwili Beki wa
Timu ya Simba,Donald Mtosi wakati mchezo wao wa Nani Mtani Jembe
unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Hadi
hivi sasa Simba wanaongoza kwa Bao 1-0 na tayari dakika 35 za mchezo
zishakatika.Picha zote na Othman Michuzi.Golikipa Machachari wa Timu ya Simba,Ivo Mapunda akiruka juu kudaka mpira uliokuwa unaelekea langini kwake.
Simba wakiandika Bao la Kwanza mnamo dakika ya 19 ya mchezo.
Mashabiki wa Simba.
Nahodha
wa Timu ya Simba,Henry Joseph Shindika akikabiliana na Mpinzani wake
wakati wa Mtanange wa Nani Mtani Jembe uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam,jioni ya leo.
Kelvin Yondani wa Yanga akitoa pasi nzuri.