Pages

Thursday, August 29, 2013

UTANDAZAJI MABOMBA YA GESI MTWARA-DAR

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya kisasa ya kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana namba tano  ya Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani .Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa  Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga Fungu, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.
 Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
 Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
 Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine
 Watalaamu wa ubora wa ufungaji mabomba ya gesi kutoka Afrika Kusini wakimueleza Waziri Muhongo kuhusu umakini wakati wa kuunganisha mabomba hayo
 Profesa Muhongo akiwa eneo la kuhifadhia mabaomba, Nyamwage, wilayani Rufiji. Mabomba hayo yalianza kuunganishwa jana.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akizungumza na baadhi ya vibarua  wa kitanzania wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya kichina katika kambi ya kuhifadhia mabomba ya Nyamwage, wilayani Rufiji, Pwani.
 Waziri Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kamapuni hiyo ya kichina.
  Kamanda Richard Mwaikenda naye akiwa katika ziara hiyo eneo la Nyamwage, Rufiji.
 Kambi ya wafanyakazi wa kamapouni ya kichina eneo la Mkuranga, Dar es Salaam
 Waandishi wa habari walioambatana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (amezibwa), wakiangalia nyaya za mkongo zitakazotandazwa sambamba na mabomba ya gesi kwa ajili ya usalama, zilizokuwa kwenye lori katika ghala la kampuni hiyo ya kichina wilayani Mkuranga, Pwani
Baadhi ya mitambo ikiwa imefungwa wilayani Mkuranga, Pwani, kwa ajili ya kuongezea unene wa mabomba maalumu ya gesi yatakayotandazwa baharini.

Serikali yaridhishwa na kasi ya ujenzi wa bomba la gesi

Serikali imeridhishwa na kasi ya kazi inayofanywa ya mradi wa kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Hayo yalibainika wakati Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa China nchini, Lu-Youging walipofanya ziara ya pamoja kukagua ujenzi wa bomba hilo. Katika ziara hiyo walitembelea kambi tano za mradi za Somangafungu, Nyamwage, Ikwiriri, Mkuranga na Kongowe katika Mto Mzinga.
Waziri Muhongo alisema ameridhishwa na kasi ya kazi inayofanywa ya mradi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam huku akiwataka watanzania kuwa na imani na kazi hiyo.
Alisema awali zoezi hilo lilitakiwa kukamilika mwezi Januari, 2015, lakini huenda likawahi kumalizika kutokana na kuwepo kwa vifaa vya kisasa na imara kutoka Kampuni ya China Petroleum Pipeline (CPP) watakao fanya kazi ya kulitandaza.
Alisema mabomba hayo ni imara na yanaweza kudumu kwa zaidi ya miaka 70 iwapo yatatunzwa vizuri na kwamba serikali itahakikisha inayafuatilia vizuri na kuhakikisha hayachafuki
Waziri Muhongo alisema kazi ya kuunganisha vipande vya bomba inaanza rasmi tarehe 26 Agosti na wakati huo uchimbaji ukiendelea kwa ajili ya kuweka mabomba hayo ambayo yatakuwa tayari yameunganishwa.
“Uunganishwaji unafanywa na mitambo ya kisasa kabisa na hapo bomba linapochimbiwa ndio hapohapo uunganishaji unafanyika na bomba zitakazolazwa baharini zitaunganishwa hukohuko” alisema.
Alisema kwa bomba zitakazoenda baharini uzito wake ni mkubwa zaidi ikilinganishwa na bomba zitazotumika nchi kavu kwakuwa zitakazolazwa baharini zitawekewa zege maalumu.
“Bomba zitakazoenda baharini zitakuwa na uzito wa zaidi ya tani 10 baada ya kuwekewa zege ambapo kwa sasa zina uzito wa tani tatu” alisema.
Alisema kazi ya kutandaza mabomba baharini itaanza Septemba 16, mwaka huu kwa kuwa kazi hiyo inahitaji umakini mkubwa.
Profesa muhongo alisema pindi bomba hilo litapokamilika uzalishaji wa umeme utaongezeka kutoka megawati 1500 zilizopo hadi kufikia megawati 3000 mwaka 2015 na kuanza kuuza umeme utakaokuwa wa ziada kwa nchi jirani.
Kuhusu suala la ajira, Waziri alisema mradi huo tayari umezalisha ajira. Alisema magari ya watanzania yapatayo 45 yamepewa kazi ya kusafirisha mabomba huku watanzania wengine wakiajiriwa katika kazi zinazoendelea.
Balozi wa China nchini, Lu Youging alisema mradi huo ni wa kipekee na una umuhimu mkubwa sana kwa uchumi wa Tanzania kwani kupitia mradi huo, Tanzania itaweza kuwa na viwanda vingi na kupelekea kuongezeka kwa ajira nchini.

Aliongeza kuwa mradi huo utasaidia katika utunzaji wa mazingira kwakuwa badala ya kuendelea kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuni, watanzania watatumia gesi asilia kwa matumizi ya kupikia.

DR Shein aendelea na ziara nchini Uholanzi



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam,Rene Van Der Plas,alipotembelea katika bandari hiyo akiwa katika Ziara ya siku tano na ujumbe wake, nchini Uholanzi,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na ujumbe wake waliokaa wakipata maelezo kutoka kwa Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,walipotembelea katika Ofisi za Bandari hiyo akiwa katika Ziara ya siku tano , nchini Uholanzi,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na ujumbe wake wakipata maelezo ya ramani ya Ujenzi wa Bandari na Mpango mzima wa utendaji kazi kutoka kwa Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas, alipotembelea katika Ofisi za Bandari hiyo akiwa katika Ziara ya siku tano nchini Uholanzi na ujumbe aliofuatana nao

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)na Mawaziri pamoja na Balozi Dr.Diadorus B. Kamala,(wa pili kulia)wakizungumza na Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,walipokuwa katika Boti walipoitembelea Bandari ya Rotterdam Nchni Uholanzi wakiwa katika ziara ya siku tano nchini humo.[

Baadhi ya Meli za Mizigo kutoka Nchi mbali mbali ikiwemo China,ni miongoni mwa Meli zinazotia nanga katika Bandari ya Rotterdam, Nchini Uholanzi kama inavyoonekana pichani ikiwa imesheheni makontena yenye Bidhaa mbali mbali.


Baadhi ya Meli za Mizigo kutoka Nchi mbali mbali ikiwemo China,ni miongoni mwa Meli zinazotia nanga katika Bandari ya Rotterdam, Nchini Uholanzi kama inavyoonekana pichani ikiwa imesheheni makontena yenye Bidhaa mbali mbali..[

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa na wawakilishi wa Makampuni yanayotaka kuwekeza Zanzibar wakiwa katika mazungumzo ya kujadili namna ya kufikia hatua za kuwekeza Nchini,wakati alipokuwa katika ziara Nchini Uholanzi itakayochukua siku tano,ambapo atatembelea sehemu kadhaa za kimaendeleo katika nchi hiyo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,walipofika katika Ofisi za Kituo hicho huko katika Bandari ya Rotterdam,nchini Uholanzi katika ziara ya siku tano.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,alipokuwa akitoa maelezo kwa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,ukioongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara nchini Uholanzi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha na Mfalme wa Uholanzi Willem Alexander,alipomtembelea katika makazi yake nchini Uholanzi,rais akiwa katika ziara ya siku tano

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wawakilishi wa Makampuni wakati alipowasili katika Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Familia ya Mfalme panoja na makampuni nchini Uholanzi akiwa katika ziara ya siku tano nchini humo. [Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]

SAMUEL ETO'O AWASILI LONDON TAYARI KUFANYIWA VIPIMO NA KUJIUNGA NA CHELSEA - MOURINHO AKIKIRI KUMSHINDWA ROONEY.

Full steam ahead: Samuel Eto'o arrived at St Pancras station on Wednesday night ahead of his move to Chelsea
Samuel Eto'o akiwasili London usiku wa jana

Chelsea inakaribia kumsajili mshambuliaji Samuel Eto’o kwa dili la mwaka mmoja lenye thamani ya £7million kwa mkataba wa mwaka mmoja leo Alhamisi baada ya kukiri kushindwa kumpata mshambuliaji wa  Manchester United Wayne Rooney.
Eto’o, 32, amekubali kupunguza dau lake alilokuwa akilipwa na Anzhi kiasi cha £17m kwa mwaka na sasa atasaini atasaini akiwa huru. 

Pamoja na hilo, lakini inaeleweka kwamba Anzhi wamemlipa Eto'o millioni kadhaa ili kuweza kumuondoa katika listi wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ndaniya klabu ya Anzhi.
Eto'o aliwasili jijini London jana usiku na anategemewa kufanyiwa vipimo vya afya mchana wa leo katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham.
London calling: Eto'oChelsea bound: Cameroon striker Eto'o arrives at St Pancras

Wednesday, August 14, 2013

SEREKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IKO KATIKA MKAKATI YA KUIFANYA HOSPITALI MNAZI MMOJA KUWA YA RUFAA


WANANCHI  wakiwa nje ya mlango kuu wa kuingia hospitali Kuu ya Mnazi mmoja, wakisubiri kupata ruhusa ya kuingia ndani ya jengo hilo kuonana na Madaktari, utaratibu huu umekuwa usumbufu kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo, kupata huduma muhumu, kutokana na usumbufu wanaopata kutoka kwa walinzi wa hospitali hiyo
 

KUNDI LA BOKO HARAMU LATISHIA MAISHA YA WATU NIGERIA

boko_haram
Wakazi wa mji wa Konduga kaskazini mwa Nigeria wametoroka baada ya wapiganaji waliovalia sare za jeshi kuwapiga risasi na kuwaua karibu watu 50 katika msikiti mmoja wa eneo hilo, muda mfupi kabla ya sala ya asubuhi.
Shambulio hilo limedaiwa kufanywa na kundi lenye itikadi kali za kiislamula  Boko Haram, ambalo linalaumiwa kwa mauaji ya mamia ya wakazi wa eneo hilo.
Shirikaka la Habari la Deutche Press limesema wafuasi 20 wa kundi la Boko Haram wanahojiwa na polisi kuhusiana na mauaji hayo

MAOFISA WA MAN UNITED NDANI YA JIJI LA MADRID KUFANYA MAZUNGUMZO YA KUMSAJILI LUKA MODRIC


Maofisa wa Manchester United wapo jijini Madrid kuzungumza na klabu ya Real Madrid kuhusu uwezakano wa kumnunua kiungo Luka Modric kwa mujibu wa mtandao wa ESPN.

Kiungo huyo mwenye miaka The 27 alihamia Spain akitokea Tottenham Hotspur kwa ada ya uhamisho wa £33 million lakini amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha Madrid, hata kufikia kupigiwa kura na mashabiki kuwa mchezaji mbovu zaidi kuwahi kusajiliwa na Madrid kwa msimu uliopita - ilikuwa mwezi January.

Alijitahidi na kucheza vizuri hasa kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya zaidi kwenye mchezo wa mtoano dhidi ya Man United katika uwanja wa Old Trafford lakini hatma yake ndani ya Madrid imezidi kuwa shakani baada ya klabu hiyo ya Spain kuongeza viungo watatu baada ya lile lundo la mwanzo - wamemsajili Isco,  Asier Illarramendi na Casemiro.

Modric kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kujiunga na United lakini mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy hakutaka kumuuza mchezaji huyo kwa wapinzani wa ligi ya nyumbani na hivyo akauzwa kwa klabu ya nje ya nchi. Kwa hali ilivyo sasa ndani ya Madrid inaweze kuwa rahisi kwa United kumpata kiungo huyo wa wa Croatia.