Pages

Tuesday, May 12, 2015

WAUGUZI ZANZIBAR WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI 12 MEI


Add caption
Wauguzi wa Zanzibar wameungana na wauguzi duniani kusherehekea siku ya wauguzi. Kauli mbiu ya mwaka huu ni ''Wauguzi chachu ya mabadiliko: huduma bora kwa gharama nafuu''. Siku hii huadhimishwa kimataifa kumkumbuka mwanzilishi wa fani ya uuguzi duniani Florence Nightingale kwa mchango wake mkubwa katika kuhudumia wagonjwa. Katika hoteli ya Bwawani wauguzi hao walihutubiwa an mwenyekiti wa baraza wa wauguzi na wakunga Bi Amina Abdulkadir aliwakumbusha wauguzi wajibu katika kuhudumia wagojwa ikiwa ni pamoja na kutunza siri za wagonjwa, kutowanyanyasa, kutokuwadhuru kwa namna yeyote ile, na nyenginezo. Katibu mkuu wa wizara ya afya amewaeleza wauguzi kuwa kero zao zinashughulikiwa na serekali. Kwa niaba ya mgeni rasmi mama Shein, naibu waziri wa habari aliwaasa wauguzi kuwapa ushirikiano wagonjwa pamoja na kuwajali. 

No comments:

Post a Comment