Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu. (Picha zote na Happiness Mnale)
Askari wa Kikosi cha
kutuliza Ghasia (FFU) wakimwingiza katika gari muumini wa Kiislamu aliyekamatwa
katika viunga vya maeneo ya Ikulu
Barabara
ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na
Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo
Polisi
wakifanya doria kwa kutumia pikipiki
Mitaa ya
Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo
Ulinzi
uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo
leo
Wanajeshi
wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leo
Askari
wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa
wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la
Kariakoo
Magari ya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara ya Msimbazi
ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka
kuandamana.
Watu hao walifika mmoja
mmoja maeneo ya Ikulu kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza
Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao
kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa
dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya
maandamano.
Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha. Katika maeneo ya Kariakoo vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania vimekuwa vikifanya doria ili kuimarisha hali ya ulinzi