Wakati Zanzibar Sakata la Waislamu kuendeleza kitimtim kufuatia kutoonekana kwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho Vurugu zimeendelea kutawala eneo la Darajani na kusababisha Polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya watu.
Jijini Dar es Salaam hali si tofauti na hiyo maeneo ya Kariakoo maduka kadhaa yamefungwa kufuatia vurugu kama hizo baada ya Swala ya Ijumaa kufuatia pia kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda yamekuwa ni matokeo ya vurugu watu kukimbizana huku Polisi wakidhibiti Usalama na Amani kuelekea harijojo.(Picha na Maktaba).
Maeneo ya Posta karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani Askari wameweka utepe wa kudhibiti watu kuingia katika maeneo hayo kitendo kilichosababisha shughuli nyingi kusimama.
Pichani ni Jeshi la Wananchi Tanzania likiwasilia maeneo ya Kariakoo kuongezea nguvu kwa ajili ya kutuliza ghasia. (Picha hii imepigwa na mdau Mpeli Jr Ngonywike kupitia mtandao wa facebook alipopiga picha hii kwa kujificha.
Baadhi ya waumini wanaodaiwa kutoka kikundi cha dini ya kiislamu wakidhibitiwa eneo la jirani na geti la Ikulu..mapema leo ambapo jumla ya watu 6, walikamatwa.(Picha na Andrew Chale).
Pichani ni maeneo ya Kariakoo magari ya jeshi JWTZ zaidi ya 8 yakiwa katika doria maeneo ya Kariakoo.
No comments:
Post a Comment