Siku chache baada ya kufutwa kazi ya kuiongoza timu ya Young Africans ya nchini Tanzania, Kocha Tom Saintfiet raia wa Ubelgiji amepata ajira mpya ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Yemen.
Tom alifutwa kazi na timu ya Yanga baada ya timu hiyo kuanza vibaya katika michuano ya ligi kuu ya Vodacom licha ya kuisaidia kutwaa taji la mashindano ya kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
Saintfiet, ambaye aliwahi kuwa kocha wa Ethiopia ameanza kazi siku ya Jumamosi na ataiongoza timu yake mpya dhidi ya Lebanon katika mechi ya kirafiki iliyopangwa kufanyika Oktoba 16.
No comments:
Post a Comment