Pages

Saturday, June 8, 2013

CHUO CHA AFYA MBWENI BINGWA WA VYUO ZANZIBAR


 .  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi kikombe cha ushindi kwa timu ya Chuo cha Afya Mbweni, baada ya kupata ushindi katika mashindano ya Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE). Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Haji Mwita.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikagua timu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu, wakati ikijiandaa kuvaana na timu ya Afya Mbweni, katika fainali za mashindano ya Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE) iliyofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikagua kikosi cha timu ya Chuo cha Afya Mbweni, wakati ilijiandaa kuvaana na timu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu, katika fainali za mashindano ya Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE) iliyofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
 Mashabiki mbali mbali waliojitokeza katika mchezo wa fainali za mashindano ya Vyuo vikuu na Taasisi za elimu Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
 Mashabiki mbali mbali waliojitokeza katika mchezo wa fainali za mashindano ya Vyuo vikuu na Taasisi za elimu Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
 Maandamano ya Taasisi za elimu ya juu Zanzibar yakipita mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, katika shamra shamra za fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika viwanja vya Amaan.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akipokea maandamano ya Taasisi za elimu ya juu Zanzibar, katika shamra shamra za fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika viwanja vya Amaan.

No comments:

Post a Comment