Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi
wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya kisasa ya
kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana namba tano ya
Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani
.Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa
maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar
es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na
baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya
kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa
katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya
utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga Fungu, wilayani
Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine
Watalaamu
wa ubora wa ufungaji mabomba ya gesi kutoka Afrika Kusini wakimueleza
Waziri Muhongo kuhusu umakini wakati wa kuunganisha mabomba hayo
Profesa Muhongo akiwa eneo la kuhifadhia mabaomba, Nyamwage, wilayani Rufiji. Mabomba hayo yalianza kuunganishwa jana.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akizungumza na
baadhi ya vibarua wa kitanzania wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya
kichina katika kambi ya kuhifadhia mabomba ya Nyamwage, wilayani Rufiji,
Pwani.
Waziri Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kamapuni hiyo ya kichina.
Kamanda Richard Mwaikenda naye akiwa katika ziara hiyo eneo la Nyamwage, Rufiji.
Kambi ya wafanyakazi wa kamapouni ya kichina eneo la Mkuranga, Dar es Salaam
Waandishi
wa habari walioambatana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (amezibwa), wakiangalia nyaya za mkongo
zitakazotandazwa sambamba na mabomba ya gesi kwa ajili ya usalama,
zilizokuwa kwenye lori katika ghala la kampuni hiyo ya kichina wilayani
Mkuranga, Pwani
Baadhi
ya mitambo ikiwa imefungwa wilayani Mkuranga, Pwani, kwa ajili ya
kuongezea unene wa mabomba maalumu ya gesi yatakayotandazwa baharini.
Serikali yaridhishwa na kasi ya ujenzi wa bomba la gesi
Serikali imeridhishwa na kasi ya kazi inayofanywa ya mradi wa kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Hayo
yalibainika wakati Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo na Balozi wa China nchini, Lu-Youging walipofanya ziara ya
pamoja kukagua ujenzi wa bomba hilo. Katika ziara hiyo walitembelea
kambi tano za mradi za Somangafungu, Nyamwage, Ikwiriri, Mkuranga na
Kongowe katika Mto Mzinga.
Waziri
Muhongo alisema ameridhishwa na kasi ya kazi inayofanywa ya mradi wa
bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam huku
akiwataka watanzania kuwa na imani na kazi hiyo.
Alisema
awali zoezi hilo lilitakiwa kukamilika mwezi Januari, 2015, lakini
huenda likawahi kumalizika kutokana na kuwepo kwa vifaa vya kisasa na
imara kutoka Kampuni ya China Petroleum Pipeline (CPP) watakao fanya
kazi ya kulitandaza.
Alisema
mabomba hayo ni imara na yanaweza kudumu kwa zaidi ya miaka 70 iwapo
yatatunzwa vizuri na kwamba serikali itahakikisha inayafuatilia vizuri
na kuhakikisha hayachafuki
Waziri
Muhongo alisema kazi ya kuunganisha vipande vya bomba inaanza rasmi
tarehe 26 Agosti na wakati huo uchimbaji ukiendelea kwa ajili ya kuweka
mabomba hayo ambayo yatakuwa tayari yameunganishwa.
“Uunganishwaji
unafanywa na mitambo ya kisasa kabisa na hapo bomba linapochimbiwa ndio
hapohapo uunganishaji unafanyika na bomba zitakazolazwa baharini
zitaunganishwa hukohuko” alisema.
Alisema
kwa bomba zitakazoenda baharini uzito wake ni mkubwa zaidi
ikilinganishwa na bomba zitazotumika nchi kavu kwakuwa zitakazolazwa
baharini zitawekewa zege maalumu.
“Bomba
zitakazoenda baharini zitakuwa na uzito wa zaidi ya tani 10 baada ya
kuwekewa zege ambapo kwa sasa zina uzito wa tani tatu” alisema.
Alisema kazi ya kutandaza mabomba baharini itaanza Septemba 16, mwaka huu kwa kuwa kazi hiyo inahitaji umakini mkubwa.
Profesa
muhongo alisema pindi bomba hilo litapokamilika uzalishaji wa umeme
utaongezeka kutoka megawati 1500 zilizopo hadi kufikia megawati 3000
mwaka 2015 na kuanza kuuza umeme utakaokuwa wa ziada kwa nchi jirani.
Kuhusu
suala la ajira, Waziri alisema mradi huo tayari umezalisha ajira.
Alisema magari ya watanzania yapatayo 45 yamepewa kazi ya kusafirisha
mabomba huku watanzania wengine wakiajiriwa katika kazi zinazoendelea.
Balozi
wa China nchini, Lu Youging alisema mradi huo ni wa kipekee na una
umuhimu mkubwa sana kwa uchumi wa Tanzania kwani kupitia mradi huo,
Tanzania itaweza kuwa na viwanda vingi na kupelekea kuongezeka kwa ajira
nchini.
Aliongeza
kuwa mradi huo utasaidia katika utunzaji wa mazingira kwakuwa badala ya
kuendelea kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuni, watanzania watatumia
gesi asilia kwa matumizi ya kupikia.