Pages

Monday, May 28, 2012

AMANI ZANZIBAR KWANZA HALAFU MAMBO MENGINE BAADAE.

 Mashehe na viongozi wa jumuiya uamsho na mihadhara ya kiislamu wakisikiliza kwa makini jambo fulani likizungumzwa.Kila kitu kinazungumzika kwenye maridhiano.Tunawaomba mashehe wetu pamoja na Wazanzibar wote kwa ujumla wetu tuweze kudumisha utulifu na amani ya nchi yetu kweni inaonekana tunakotoka kuelekea ni kubaya zaidi. Tutulie tuanadae taratibu mzuri kabisa za kupeleka hayo madai na uhakaika kabisa vyombo husika vitayasikiliza, kwa undani wake na kufikia muafaka, kuliko kuendelea na vurugu mwisho wako ni kutofikia makubaliano, naamini kuwa Mwenyezi Mungu atatujaalia imani, busara, hekima na maridhiano.
Viongozi wa Jumuiya za Sekta ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, akizungumzia hali iliojitokeza juzi ya fujo katika mitaa ya Mji wa Zanzibar. na kulani hali hiyo.isitokee tena ikaharibu Amani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinasifika kwa Amani katika Afrika Mashariki.
Mkuu wa jeshi la polisi Tanzani IGP Said M wema akizungumza na mashehe
na wadau wengine, pembeni ni waziri wa mambo ya mbani ya nchi na kamishna wa polisi Zanzibar.
Mussa Ali Mussa

HALI YA AMANI ZANZIBAR YAZIDI KUIMARIKA.
Maeneo ya mji wa Zanzibar yakiwa katika harakati za kuweka ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.Jeshi la polisi likifanya jukumu lake kuimarisha ulinzi na usalama

No comments:

Post a Comment