Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais, Mohd Aboud. |
Kamishna mkuu wa jeshi la polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa.. |
Taarifa ya SMZ
ya matukio ya uvunjifu wa amani
Posted
on May 27, 2012 by zanzibaryetu
Aidha,
serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo
vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka pale ambapo wana
maoni yoyote kuhusu serikali wafuate taratibu zilizowekwa na serikali itakuwa
tayari kuzungumza nao ili kuwa na mustakabali mwema katika nchi yetu. Vile
vile, kupitia taarifa maalumu ya serikali iliyotolewa Aprili Mei mwaka huu
serikali ilieleza wazi kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi
na kuwataka wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya
kutaka kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria
namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka huu
2012.
Taarifa
rasmi ya serikali kwa wananchi kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani nchini
Itakumbukwa
kwamba tarehe 25 Aprili, 2012 Kamati Maalumu ya Mawaziri ilikutana na viongozi
wa jumuiya ya Uamsho, Maimamu na Masheikh kuzungumzia hali iliyojitokeza nchini
katika kufanya mihadhara ambayo ilikuwa inaashiria uvunjifu wa amani.
Katika
kikao hicho serikali iliwataka viongozi hao wanapofanya mihadhara na mikutano
inayohusu masuala ya maoni ya katiba wafuate taratibu zilizowekwa kisheria.
Aidha,
serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo vinavyoashiria
uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka pale ambapo wana maoni yoyote
kuhusu serikali wafuate taratibu zilizowekwa na serikali itakuwa tayari
kuzungumza nao ili kuwa na mustakabali mwema katika nchi yetu.
Vile
vile, kupitia taarifa maalumu ya serikali iliyotolewa Aprili Mei mwaka huu
serikali ilieleza wazi kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi
na kuwataka wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya
kutaka kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria
namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka huu
2012.
Kwenda
kinyuma na sheria hii ni kosa la jinai na hivyo iliwataka wananchi wote
kujiepusha na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na matakwa ya sheria.
Ndugu
wananchi mbali na juhudi hizo za serikali bado wapo watu wachache wasioitakia
mema nchi yetu na umoja uliopo wanaendeleza kwa makusudi vitendo vya kuvunja
taratibu za sheria jambo ambalo limepelekea jeshi la polisi kuchukua hatua za
kisheria.
Ndugu
wananchi serikali imesikitishwa na vitendo vilivyojitokeza vya vurugu na
uvunjifu wa amani ambavyo vimeelezwa kwa kina na jeshi la polisi iliyotolewa
mapema leo tarehe 25.05.2012 na kamishana wa polisi zanzibar.
Kutokana
na hali hiyo serikali inawahakikishia wananchi wote kwamba itaendelea kudhibiti
vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria vinavyoashiria kuondolea nchi yetu
amani na utulivu uliopo.
Ndugu
wananchi serikali inawahakikishia wananchi kwamba jeshi la polisi litaendelea
kuchukua hatua zifaazo ili kuwahakikishia usalama wa raia na mali zao unakuwepo
na hali inaendelea kuwa shuwari amani na utulivu.
Ndugu
wananchi bado serikali inasisitiza na kuwaomba wananchi wote waunge mkono
juhudi za serikali na kuwacha kabisa kujiingiza katika vitendo ambavyo vinaashiria
uvunjifu wa amani na utulivu katika nchi yetu.
Hivyo
tunawaomba wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida na serikali
itaendelea kuwahakikishia usalama wao.
Aidha
serikali inawaomba wazazi kuwadhibiti vijana wao wasijiingize katika vitendo
viovu na vurugu kwani jeshi la polisi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama
vitakuwa macho kupambana na vurugu hizo na vitendo vyote vya uvunjifu wa amani.
Kwa
madhumuni ya kudhibiti amani na utulivu na usalama wa wananchi wetu serikali
katika kipindi hiki itachukua hatua zifuatazo:
1.
Inakataza mikusanyiko ya aina mbali mbali, maandamano, na mihadhara ya aina
mbali mbali ambayo haijapata kibali cha serikali.
2. Serikali inaliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na kufanya fujo zilizotokea katika maeneo mbali mbali ya zanzibar
3. serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa amali zilizofanywa katika taasisi za umma, dini na mali za watu binafsi.
4. Serikali inawapa pole wananchi na taasisi zilizoathirika na vurugu hizo na kuwahakikishia kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika katiak kadhia hiyo.
Na mwisho tunawaomba wananchi kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale ambapo itaonekana zipo dalili za uvunjifu wa amani katika maeneo yao.

Ahsanteni
Nawashukuru
kwa kunisikiliza.
Mohammed
Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.
No comments:
Post a Comment