Pages

Monday, September 10, 2012

MANCHESTER UNITED AND MANCHESTER CITY, ARSENAL, LIVEPOOL KUMUWANIA FELLAINI



Maroune Fellaini amesema kwamba muda wake wa kukaa Goodson Park umefikia tamati.

Kiungo huyo mwenye miaka 24 raia wa Ubelgiji bado yupo kwenye mkataba wa miaka minne na Everton, lakini alisema: "Ndio nimeanza msimu wangu wa tano na Everton, huu utakuwa wa mwisho hapa.

"Nimeshaona kila kitu. Mwezi January au mwishoni mwa msimu nitaondoka hapa na kujiunga klabu nyingine."

Baada ya kauli hii Fellaini ambaye tayari ameshaichezea Klabu ya Merseyside mechi 130 na kufunga mabao 22.


Kauli hii ya Fellaini kwa hakika itaanzisha vita ya mapema ya kugombea saini yake baina ya vilabu vikubwa nchini England. Kati ya Manchester United, Manchester City au Liverpoool na Chelsea - unadhani wapi ni mahali sahihi na kwanini ajiunge na timu hiyo.

No comments:

Post a Comment