Wizara ya Ulinzi ya
Ufaransa inasema kuwa jeshi linaloongozwa na Wafaransa limeuteka uwanja wa ndege
wa mji wa Gao, ngome ya wapiganaji ya Kiislamu kaskazini mwa Mali.Daraja muhimu piya
wameiteka. Mapigano
yanaendelea. Gao ni mmoja kati ya miji mikuu mitatu ya kaskazini mwa Mali iliyotekwa na wapiganaji mwaka jana. Siku ya Ijumaa wanajeshi wa Mali na Ufaransa waliukomboa mji wa Hombor kilomita 160 kutoka Gao. Umoja wa Afrika umesema unataka kuzidisha idadi ya wanajeshi wa kuweka amani nchini Mali, na imeomba nchi zanachama kujitolea kwa wanajeshi zaidi katika wiki zijazo. Piya umeuomba Umoja wa Mataifa usaidie kuwasafirisha wanajeshi hao hadi Mali. |
Sunday, January 27, 2013
MALI UNREST.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment