Pages

Thursday, May 31, 2012

Diamond On Stage

WILFRED AWASILI MKOANI KILIMANJARO

WILFRED AWASILI MKOANI KILIMANJARO:   W ilfred Moshi ambaye ni Mtanzania wa kwanza kufika kilele cha mlima mrefu kiliko yote duniani amewasili jana saa saba mchana Nchini. ...

CITY SPORTS LOUNGE SIKU UFUNGUZI!!!

CITY SPORTS LOUNGE SIKU UFUNGUZI!!!: Naibu waziri wa Mawasiliano akisalimiana na Juma Pinto Siku ya Ufunguzi wa City Sports Lounge, picha za wananchi mbali mbali wali...

Serikali Italinda Amani kwa Nguvu Zote - Dk Shein

Serikali Italinda Amani kwa Nguvu Zote - Dk Shein: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein ,alipokuwa akizungumza na Wahariri na Waandishi wa habari wa v...

WABUNGE WA CHADEMA ZIARANI NCHINI MAREKANI WAAGWA ...

 WABUNGE WA CHADEMA ZIARANI NCHINI MAREKANI WAAGWA ...: Baaada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha tawi la chadema Washington Dc Maryland na Virginia,Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maen...

Wednesday, May 30, 2012

Mji wa Zanzibar Ukiwa katika Amani na Utulivu.

Mji wa Zanzibar Ukiwa katika Amani na Utulivu.:  Watalii wanaotembelea Mji wa Zanzibar wakiwa katika hali ya amani na utulivu wakitembelea maeneo ya Mji Mkongwe kujionea sehemu za histo...

Monday, May 28, 2012

AMANI ZANZIBAR KWANZA HALAFU MAMBO MENGINE BAADAE.

 Mashehe na viongozi wa jumuiya uamsho na mihadhara ya kiislamu wakisikiliza kwa makini jambo fulani likizungumzwa.Kila kitu kinazungumzika kwenye maridhiano.Tunawaomba mashehe wetu pamoja na Wazanzibar wote kwa ujumla wetu tuweze kudumisha utulifu na amani ya nchi yetu kweni inaonekana tunakotoka kuelekea ni kubaya zaidi. Tutulie tuanadae taratibu mzuri kabisa za kupeleka hayo madai na uhakaika kabisa vyombo husika vitayasikiliza, kwa undani wake na kufikia muafaka, kuliko kuendelea na vurugu mwisho wako ni kutofikia makubaliano, naamini kuwa Mwenyezi Mungu atatujaalia imani, busara, hekima na maridhiano.
Viongozi wa Jumuiya za Sekta ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, akizungumzia hali iliojitokeza juzi ya fujo katika mitaa ya Mji wa Zanzibar. na kulani hali hiyo.isitokee tena ikaharibu Amani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinasifika kwa Amani katika Afrika Mashariki.
Mkuu wa jeshi la polisi Tanzani IGP Said M wema akizungumza na mashehe
na wadau wengine, pembeni ni waziri wa mambo ya mbani ya nchi na kamishna wa polisi Zanzibar.
Mussa Ali Mussa

HALI YA AMANI ZANZIBAR YAZIDI KUIMARIKA.
Maeneo ya mji wa Zanzibar yakiwa katika harakati za kuweka ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.Jeshi la polisi likifanya jukumu lake kuimarisha ulinzi na usalama

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Akutana na Viongozi wa Di...

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Akutana na Viongozi wa Di...: Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk.Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Viongozi wa Jumuiya za Kiislam na Wadau wac Sekta ya Utalii Zanziba...

: Hali Ilivyokuwa Usiku na Mchana wa Jana katika Mi...

Van Persie won’t say yes to Arsenal until they bring in top players

Van Persie won’t say yes to Arsenal until they bring in top players

TWIGA STARS WAGONGWA 2-1 NA ETHIOPIA

 TWIGA STARS WAGONGWA 2-1 NA ETHIOPIA: Twiga Stars TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imeanza vibaya kampeni za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la ...

Ghasia za sababisha uharibifu wa mali Zanzibar

Ghasia za sababisha uharibifu wa mali Zanzibar

Hali Ilivyokuwa Usiku na Mchana wa Jana katika Mi...

Sunday, May 27, 2012

Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais, Mohd Aboud.
Kamishna mkuu wa jeshi la polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa..

Taarifa ya SMZ ya matukio ya uvunjifu wa amani

Posted on May 27, 2012 by zanzibaryetu

Aidha, serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka pale ambapo wana maoni yoyote kuhusu serikali wafuate taratibu zilizowekwa na serikali itakuwa tayari kuzungumza nao ili kuwa na mustakabali mwema katika nchi yetu. Vile vile, kupitia taarifa maalumu ya serikali iliyotolewa Aprili Mei mwaka huu serikali ilieleza wazi kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi na kuwataka wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya kutaka kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka huu 2012.

Taarifa rasmi ya serikali kwa wananchi kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani nchini

Itakumbukwa kwamba tarehe 25 Aprili, 2012 Kamati Maalumu ya Mawaziri ilikutana na viongozi wa jumuiya ya Uamsho, Maimamu na Masheikh kuzungumzia hali iliyojitokeza nchini katika kufanya mihadhara ambayo ilikuwa inaashiria uvunjifu wa amani.

Katika kikao hicho serikali iliwataka viongozi hao wanapofanya mihadhara na mikutano inayohusu masuala ya maoni ya katiba wafuate taratibu zilizowekwa kisheria.

Aidha, serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka pale ambapo wana maoni yoyote kuhusu serikali wafuate taratibu zilizowekwa na serikali itakuwa tayari kuzungumza nao ili kuwa na mustakabali mwema katika nchi yetu.

Vile vile, kupitia taarifa maalumu ya serikali iliyotolewa Aprili Mei mwaka huu serikali ilieleza wazi kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi na kuwataka wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya kutaka kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka huu 2012.

Kwenda kinyuma na sheria hii ni kosa la jinai na hivyo iliwataka wananchi wote kujiepusha na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na matakwa ya sheria.

Ndugu wananchi mbali na juhudi hizo za serikali bado wapo watu wachache wasioitakia mema nchi yetu na umoja uliopo wanaendeleza kwa makusudi vitendo vya kuvunja taratibu za sheria jambo ambalo limepelekea jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria.

Ndugu wananchi serikali imesikitishwa na vitendo vilivyojitokeza vya vurugu na uvunjifu wa amani ambavyo vimeelezwa kwa kina na jeshi la polisi iliyotolewa mapema leo tarehe 25.05.2012 na kamishana wa polisi zanzibar.

Kutokana na hali hiyo serikali inawahakikishia wananchi wote kwamba itaendelea kudhibiti vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria vinavyoashiria kuondolea nchi yetu amani na utulivu uliopo.

Ndugu wananchi serikali inawahakikishia wananchi kwamba jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua zifaazo ili kuwahakikishia usalama wa raia na mali zao unakuwepo na hali inaendelea kuwa shuwari amani na utulivu.

Ndugu wananchi bado serikali inasisitiza na kuwaomba wananchi wote waunge mkono juhudi za serikali na kuwacha kabisa kujiingiza katika vitendo ambavyo vinaashiria uvunjifu wa amani na utulivu katika nchi yetu.

Hivyo tunawaomba wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida na serikali itaendelea kuwahakikishia usalama wao.

Aidha serikali inawaomba wazazi kuwadhibiti vijana wao wasijiingize katika vitendo viovu na vurugu kwani jeshi la polisi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vitakuwa macho kupambana na vurugu hizo na vitendo vyote vya uvunjifu wa amani.

Kwa madhumuni ya kudhibiti amani na utulivu na usalama wa wananchi wetu serikali katika kipindi hiki itachukua hatua zifuatazo:

1. Inakataza mikusanyiko ya aina mbali mbali, maandamano, na mihadhara ya aina mbali mbali ambayo haijapata kibali cha serikali.
2. Serikali inaliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na kufanya fujo zilizotokea katika maeneo mbali mbali ya zanzibar
3. serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa amali zilizofanywa katika taasisi za umma, dini na mali za watu binafsi.
4. Serikali inawapa pole wananchi na taasisi zilizoathirika na vurugu hizo na kuwahakikishia kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika katiak kadhia hiyo.
Na mwisho tunawaomba wananchi kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale ambapo itaonekana zipo dalili za uvunjifu wa amani katika maeneo yao.

Ahsanteni

Nawashukuru kwa kunisikiliza.

Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.


Barry injury only concern for satisfied Hodgson

Barry injury only concern for satisfied Hodgson

Usiku wa kuamkia leo hali ilikuwa hivi, lakini Mungu atujalie imani ili tusifike kubaya zaidi Wazanzibar ni watu waungwana na watiifu kunako mambo. Inasemekana na  habari zisizo na uhakika kwamba baadhi ya viongozi wa jumuiya wamekamatwa,lakini hakuna chombo kilichothibitisha halii hii.

Dozens of children killed in new Syria attack

Dozens of children killed in new Syria attack


Askari wa kutuliza ghasia [FFU] wakizunguka katika mji wa Zanzibar kuhakikisha kwamba, hali inakuwa shwari na shughuli kurudi katika hali ya kawaida.
. Sehemu za Michenzani inavyoonekana katika picha hii jinsi, ilivyo, hii ni katikati ya mji wa Zanzibar.Mungu ibariki Zanzibar na watu wake wote,sisi tunaomba amani tu itawale.

Saturday, May 26, 2012


Baadhi wa wanawake wa kiislamu wa Zanzibar wakiandamana  kwa amani barabarani pamoja na Jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar,wakiishindikiza serekali ya Zanzibar na Muungano juu ya uhuru wa Wazanzibar.Hii inaonesha jinsi gani wananchi wanauelewa juu mbabo yao, yanayowahusu. Kila mtu ana haki ya kikatiba juu ya maamuzi ya nchi yake.