KIZAZAA CHAENDELEA AFGHANISTAN; WATU KADHAA WAUAWA KATIKA MILIPUKO YA KUJITOA MHANGA.
Watu kadhaa wameuawa Kusini-Magharibi mwa Afghanistan katika mfululizo wa mashambulizi ya kujitoa mhanga.
Maafisa waandamizi wa polisi katika jimbo la Nimroz wamesema takriban maeneo manne tofauti yameshambuliwa katika mji mkuu wa jimbo hilo wa Zaranj.
Takriba watu 35 wameuawa na wengine karibia 80 wamejeruhiwa.
Mlipuko umetokea katika soko ambapo watu kadhaa walikuwa katika heka heka za kujiandaa kusherehekea kumalizika kwa mfungo wa mwezi Ramadan.
Naibu Mkuu wa Polisi wa Jimbo hilo Mujibullah Latifi amekaririwa akisema baadhi ya washambulizi hao wameuawa na polisi.
No comments:
Post a Comment