Moussa Konate ndiye aliyeisawazishia timu yake ya Senegal baada ya United Arab Emirates kutangulia kupata goli la kwanza kupitia mchezaji wake Ismaeil Matar.
Moussa anayo nafasi nzuri yakuondoka na kiatu cha dhahabu kutokana na kufunga magoli yote manne ya Senegal hadi hivi sasa.
Katika hatua ya robo fainali Senegal itakutana na Mexico baada ya Mexico kuifunga Switzerland goli 1-0 na hivyo kushikilia uskani wa kundi B.
Nayo timu ya Misri imefanikiwa kutinga hatua hiyo ya robo fainali baada ya kuifunga Belarus goli 3-1 na sasa watapambana na Japan siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Old Trafford.
No comments:
Post a Comment