MABAKI YA HELKOPTA ZA UGANDA ZILIZOPOTEA YAPATIKANA NCHINI KENYA BAADA YA KUANGUKA
Mabaki ya helkopta mbili za Uganda zilizokuwa zimepotea yameonekana nchini Kenya katika maene ya Mlima Kenya baada ya kuanguka.
Kwa mujibu wa Afisa wa Kijeshi wa Kenya hatma ya watu 10 waliokuwa wakisafiri na helkopta hizo bado haijulikani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kenya, helkopta hizo zipatikana moja ikiwa imeungua kabisa na nyingine ikining’inia kwenye mwamba.
Helkopta hizo mbili zilikuwa ni sehemu ya kikosi kulichokuwa kinakwenda kuongeza nguvu katika majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika yaliyoko Somalia.
Awali helikopta 4 ziliondoka na kupaswa kusimama nchini Kenya, lakini kwa mshangao ni helkopta 1 tu ilitua salama.
Helkopta ya 4 katika kundi hilo pia imeanguka, lakini watu wote 7 waliokuwa ndani yake wameokolewa.
Helkopta hizo zilizokuwa zimepotea mabaki yake yalipatikana na Maafisa Huduma za Wanyamapori wa Kenya.
Kwa sasa jeshi la Kenya linaendelea na zoezi la kuokoa, japokuwa wamesema mahali zilipoangukia hapafikiki kirahisi hivyo inawabidi kutumia utaamu na askari wa miguu, kwa ku eneo zilipo hakuna sehemu ya kutua.
No comments:
Post a Comment