Wasiolipa ada kutofanya mitihani SUZA
Kiongozi wa Serekali ya Wanafunzi akimuunesha
orodha ya Wanafunzi ambao majina yao yanasubiri malipo yao kutoka Bodi ya Mkopo
ya Elimu ya Juu .
Wanafunzi wa Chuo Kikuu ch Taifa Zanzibar SUZA,
wakiwa nje ya Ofisi ya Mhasibu wa Chuo wakisubiri hatma yao, kuweza kufanya
mitihani yao inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Wasiolipa ada kutofanya mitihani SUZA
Na Mwanajuma Mmanga
UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimezuwiya kufanya mitihani kwa wanafunzi wote ambao hawajakamilisha ada za masomo hali ambayo imepelekea mgongano na mizozo baina ya wanafunzi na uongozi wa chuo hicho.
Kauli hiyo imetolewa na wanafunzi wa chuo hicho
walipokuwa katika maandamano ya kudai haki yao kufanya mitihani hiyo.
Mmoja miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho Ali
Kombo alisema wiki moja baadae tunatarajia kufanya mitihani hiyo ghafla
wanapokea taarifa ya kuwa kila mwanafunzi hajakamilisha malipo ya ada
hatomruhusu kufanya mtihani jambo ambalo ni kinyume na matakwa yao.
Pia alisema kuna baadhi ya wanafunzi wanalipiwa
na bodi ya mikopo la taifa lakini mpaka sasa hawajaingiziwa fedha hizo hali
ambayo inarejesha nyuma masomo yao.
"Sisi baadhi yetu tushalipiwa na bodi kwa
asilimia 90 na kumebaki asilimia 10 tu kwanini wakatuzuilia kutofanya mitihani
hiyo. hii fedha kama asilimia 80 ishalipiwa na bodi wakati hela hiyo inakuja
moja kwa moja inaingia kwenye akaunti" alisema.
Kwa upande wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa
chuo hicho Ali Sharifu Kombo, alisema kuwa yeye binafsi kwa kushirikiana na
uongozi wa serikali yake wameshafuatilia kwenye bodi ya mikopo Tanzania na
kuhakikishiwa kuwa fedha hizo tayari wameshaingiziwa.
Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Rai
alisema fedha za wanafunzi hao bado hazijaingizwa nao kama uongozi wanalalamikia
kudai ada za masomo ya wanafunzi kwa lengo la maendeleo ya chuoni hapo.
Sambamba na hilo Nae Kaimu Meneja wa Bodi ya
Mikopo Tanzania, Patric Show alisema fedha za wanafunzi hao tayari
zimeshaingiziwa katika akaunti zao na hivyo inawezekana ikawa ni kuchelewa kwa
mawasiliano baina ya bodi na Uongozi wa chuo hicho.
Meneja huyo wa bodi hiyo alisema mchakato mzima
uliosababisha kuchelewa kwa kufika barua hiyo katika bodi ya mikopo Dar es
Salaam kwa muhusika mkuu ni Sajent wa bodi, lakini kumbe kabla ya hapo Mhasibu
wa chuo hicho, Rukia tayari ameshaingiziwa tokea jana.
Kutokana na kuchelewa kwa kupelekwa kwa barua
hiyo tayari zimeshaingizwa ndani ya akaunti zao kwa kila mwanafunzi ambae yuko
chuoni hapo.
Meneja huyo amekiri kuwa fedha hizo tayari
zimeshaingizwa ndani ya akaunti hizo jumla ya shilingi milioni 13, kwa orodha ya
wanafunzi 58 wa chuo SUZA.
Hivyo amewataka wanafunzi hao kuwa
wastahamilivu katika kuvuta subra na kuwa wasikivu kwani mipango yote ishakaa
sawa na kila mmoja atapata haki yake na atafanya mtihani huo.
No comments:
Post a Comment