Maandalizi ya Sensa ya watu na makaazi yanaendelea vyema
:- Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya
Sensa Tanzania Balozi Seif Ali Iddi akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sensa
Tannzania Hajat Amina Mrisho Said wakati alipofanya ziara fupi kukagua ghala kuu
la vifaa vya Sensa liliopo Kibaha kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati hiyo.
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya
Sensa Tanzania Makamu wa Piliwa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
akikiendesha Kikao cha Tano cha Kamati hiyo kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Kibaha. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na
Mipango ya Maendeleo Zanzbar Mh. Omar Yussuf Mzee na Kulia ni Naibu Waziri wa
Fedha wa Muungano Mh. Saada Mkuya.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linalosimamia Idadi ya Watu { UNFPA } Bibi Mariam Khan akiwasailisha salamu za
Shirika hilo katika Kikao cha Tano cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania
kilichokutana Ofisi ya Mkuu a Mkoa Kibaha chini ya Mwenyekiti wake Balozi Seif
Ali Iddi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Na Othman Khamis Ame
Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka
2012 Nchini yanaendelea vyema kulingana na ratiba ya utekelezaji licha ya
changamoto ndogo ndogo zilizopo hivi sasa.
Hilo lilifahamka katika Kikao cha Tano cha
Kamati Kuu ya Tifa ya Sensa ya Watu na Makazi kilichofanyika katika Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa Kibaha chini ya Mwenyekiti Mwenza wa Kmati hiyo Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Miongoni mwa changamoto zilizotajwa katika
kikao hicho ni kwa baadhi ya Viongozi wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuhamasisha
waumini wao kutoshiriki katika zoezi la sensa kwa madai ya kutoingizwa kwa swali
la Dini kwenye madodoso ya Sensa.
Akitoa Taarifa ya maandalizi ya Sensa ya Watu
na Makazi kwa upande wa Tanzania Bara Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Saada Mkuya alisema hatua za maandalizi
hayo zinaendelea na sasa zimeingia katika hatua muhimu ya kuelekea kipindi cha
kuhesabu Watu.
Mh. Saada alisema wakala wa Majengo tayari
ameshakamilisha matengenezo ya jengo la kuingizia Takwimu kwenye kompyuta
sambamba na uwekaji wa umeme kazi inayotarajiwa kukamilika Agosti 15 mwaka huu.
Alisisitiza kwamba utekelezaji wa tathmini ya
sense utaanza mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu mwezi septemba
mwaka 2012 ikitanguliwa na Kamati ya Kitaalamu ya Sensa kupitia madodoso,
miongozo na sampuli itakayotumika wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
Naibu Waziri wa Fedha wa Muungano Mh. Saada
alifahamisha kwamba Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi Bilioni 22.5 kwa ajili
ya uhamasishaji, mafunzo ya wakufunzi ngazi ya Mikoa pamoja na ununuzi na
usafirishaji wa vifaa kupelekwa Mikoani.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi
na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee alisema kwa upande wa
Zanzibar matayarisho ya Sensa yako katika hatua ya za mafunzo kuelekea kipindi
muhimu cha kuhesabu watu.
Mh. Omar alisema shughuli za uhamasishaji pia
zimefikia hatua nzuri kwa kupitia na kushirikishwa Ofisi ya Mufti Mkuu wa
Zanzibar kwa kuendelesha Mikutano na Viongozi wa Dini. Alisema shughuli hiyo pia
imekwenda sambamba na maandalizi ya matangazo, vipindi vya uhamasishaji katika
Taasisi za Habari pamoja na michezo ya kuigizwa inayoandaliwa na wasanii maafuru
nchini.
Mapema Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu { UNFPA } Bibi Mariam Khan ambae alipata
fursa ya kutoa salamu katika kikao hicho alisema Dunia wakti wote inahitaji kuwa
na Takwimu sahihi ya idadi ya watu kwa Maendeleo ya Ustawi wao Kiuchumi na
Ustawi wa Jamii.
Bibi Mariam alisema Shirika hilo litaendelea
kushirikiana na Tanzania ikiwa ni miongoni mwa Nchi 140 Duniani zinazopata
huduma kutoka shirika hilo katika harakati za makusanyo ya Takwimu ili kuwa na
uhakika wa mipango sahihi ya Maendeleo.
Mwenyekiti Mwenza wa Kikao hicho cha Kamati
Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi Balozi Seif Ali Iddi alilipongeza
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu { UNFPA } kwa hatua zake za
kuunga mkono Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Tanzania mwaka huu wa
2012.
Balozi Seif alisema hatua ya Shirika hilo hasa
katika masuala ya uwezeshaji na Taaluma imewawezesha watendaji wa Kamati ya
Sensa na zile za Takwimu bara na Zanzibar kuendelea kufanya kazi kitaalamu
zaidi.
Mapema Mwenyekiti huyo mwenza wa Kamati Kuu ya
Taifa ya Sensa Balozi Seif Ali Iddi alielezea kuridhika kwake na hali nzuri ya
Kituo kikuu cha Vifaa vya Sensa kilichopo Kibaha ambacho kinaendelea na
matengenezo ya mwisho.
Alisema kazi kubwa iliyopo hivi sasa ni kwa
viongozi kuendelea kuhamasisha Wananchi umuhimu wa kujiandaa kwa ajili ya
uandikishaji wa sense wakati za zoezi utakapowadia.
No comments:
Post a Comment