Pages

Tuesday, August 14, 2012

LAWAMA KWA RAFAEL WA MANCHESTER UNITED.

Monday, August 13, 2012

SHIRIKISHO LA SOKA LA BRAZIL LAMTUPIA LAWAMA ZA KUFUNGWA OLYMPIC RAFAEL WA MAN UNITED, KOCHA NA NEYMAR WAMTETEA

Siku mbili baada ya kushindwa kuvunja mwiko wa kutochukua medali ya dhahabu kwenye soka katika michuano ya Olympic, shirikisho la soka la Brazil limechukua hatua ya kushangaza kwa kumlaumu beki wa kimataifa wa nchi anayekipiga Manchester United Rafael kutokana na kufungwa kwenye fainali dhidi ya Mexico.

Kosa alilofanya Rafael lilipelekea Mexico kupata goli la kwanza sekunde ya 29 tu ya mchezo. Brazil walihangaika kupata goli la kusawazisha mapema lakini wakaishia kutandikwa la pili kwenye dakika ya 74.

Mshambuliaji wa Porto Hulk akasawazisha bao moja katika dakika za majeruhi lakini halikutosha kwa Brazil ambao wameshashinda medali za dhahabu za World Cup mara tano lakini hawajawahi kuigusa ya Olympic.

Shirikisho la soka la Brazil lilitoa taarifa jana likimlaumu kinda huyo mwenye miaka 21kwenye website, ambayo ilisema: "Beki wa kulia Rafael anajua alifanya makosa ambayo yamepelekea goli la kwanza kwenye mechi dhidi ya Mexico katika Olympic London 2012.
"Hakuna cha kukataa, ingawa kwa uwezo na kiwango chake, Rafael hawezi kuhukumiwa kwa kosa hilo tu"
"Makosa yapo ili yarekebishwe. Rafael anajua hili. Baadae, mambo yatakapotulia, kwa hakika ataangalia mbele na kujifunza zaidi"

Lawama hizi za shirikisho ni tofauti kabisa mtazamo wa wachezaji na makocha ambao walimtetea kinda huyo wa Sir Alex Ferguson.

Kocha Mano Menezes amesema Brazil walikuwa na dakika 89 za kusawazisha na kubadilisha matokeo lakini haikuwa hivyo, wakati Neymar alisema kila mchezaji wa timu hiyo anapaswa kubeba mzigo wa lawama.

 

No comments:

Post a Comment