WALE WA DIET MNAENDELEAJE?
Tuesday, July 31, 201218comments
Imeshapita wiki sasa toka tuanze ile diet yetu ya mwezi
mzima.Diet yetu ni ya juice kwa wingi,maji kwa wingi na mboga mboga.Nilipata
ujumbe kwa dada aliyeomba tusaidiane kupeana tips za namna ya kutengeneza juice
mbali mbali.Mie natoa kadhaa na kama unazo na wewe tuandikie hapa kwenye
maoni.
Ikumbukwe kuwa juice yetu lazima iwe nzito na isiwe na
sukari.Hapa ntakutajia aina za matunda utakazochanganya na kupata cocktail
saaafiii.
1.Nanasi
na carot unapata juice nzuri na
2.Tikiti
maji na ndizi
3.Pesheni
na parachichi
4.Embe na
limao
5.Embe na
nanasi
6.Embe,chungwa na pesheni.
Zile
siku zetu za samaki kumbuka ni samaki choma au wa
kuchemsha.
Mazoezi kama kawa ni muhimu hata kwa dk
30Kuna hii gym inaitwa AZURA nitaanza kufanya mazoezi hapo siku chache zijazo.Nimeongea na uongozi wa hapo na tumekubaliana nao mambo kadhaa.Nitatoa nafasi tatu kwa wadau wangu humu za kufanya mazoezi bure mpaka utakapo fikia malengo yako.Ni gym nzuri ya kisasa na ipo ufukweni mwa bahari maeneo ya Kawe.Tutafanya mazoezi pamoja mimi na wewe tukiwa chini ya uangalizi wao ili tupate matokeo mazuri.Tutapima afya kama kuna kisukari,blood pressure na kupewa ushauri katika maswala ya chakula.
Haya basi endelea kutembelea hapa ili upate kujua namna ya kushiriki na kushinda nafasi hii adimu na ya kipekee.
No comments:
Post a Comment